Wasimamishwa kazi kupisha uchunguzi mradi wa shule

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Omari Mgumba, amewasimamisha kazi watumishi wanne wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, ili kupisha uchunguzi wa mradi wa Shule ya Sekondari ya Bweni ya Churtur, wilayani Muheza kushindwa kukamilika kwa wakati.

Maagizo hayo ameyatoa wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo, iliyoko katika sekta ya elimu na afya wilayani humo, ambapo amebaini ubadhirifu mkubwa wa fedha kwenye mradi huo.

“Watumishi hawa naomba watupishe wakae pembeni, kwani tayari Mkurugenzi Nassib Mbaga alishasimamishwa na hawa wengine wajumuike naye, ili kupisha uchunguzi huku tukiendelea kubaini wengine waliohusika na kuwachukulia hatua stahiki,”amesema.

“Maelekezo ya serikali ilikuwa darasa lijengwe kwa Sh mil 20, lakini hapa Muheza mmejenga darasa kwa Sh mil 33, vyumba vya maabara Sh mil 50 mmejenga kwa Sh mil 91.2, huku mabweni Sh mili 80 mmejenga kwa Sh mil 225.6.

“Ubadhirifu huu siwezi kuuvumilia lazima mtupishe tufanye uchunguzi, ili kujiridhisha kwanza, kwani miradi yenu mingi imekuwa ikisuasua hadi kuongeza fedha nyingine za mapato ya ndani, wakati miradi yote imekuja na maelekezo ya matumizi ya fedha zake,” amesema.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x