WASIMAMIZI na wasimamizi wasaidizi 250 wa vituo mbalimbali vya kupigia kura wameapishwa katika Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2024.
Akizungumza wakati wa ghafla hiyo fupi ya uapisho kwa wasimamizi hao, msimamizi wa uchaguzi katika manispaa hiyo ya Mtwara Mikindani, Hassan Nyange amewahimiza wasimamizi hao kufanya kazi hiyo kwa kujituma na kwa uzalendo mkubwa ili zoezi hilo liweze kukamilika kwa amani na utulivu.
Uapisho huo umefanyika leo Novemba 23,2024 katika manispaa hiyo ambapo wasimamizi hao wamekula viapo viwili ikiwemo kiapo cha uaminifu na utunzaji wa siri pamoja na kiapo cha utii na uadilifu.
‘’Niwaombe wasimamizi, wakati wa zoezi hili la uchaguzi jambo kubwa na la msingi ni kujiamini na kuwa wasikivu wakati wote wa mafunzo ili mukaifanye kazi hii vizuri’’amesema Nyange