KAMPUNI ya Magazeti ya Serikali (TSN) imewakaribisha watafiti, wafanyabiashara na wananchi kwa ajili ya kupata habari na taarifa mbalimbali za sasa na zile za kumbukumbu tangu miaka ya 1930
Ukaribisho huo umetolewa leo Julai 5, 2023 na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara TSN, Felix Mushi ndani ya banda la TSN kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ‘Sabasaba’ 2023.
“Niwakaribishe wote katika banda letu lililopo hapa Sabasaba kwa ajili ya kutangaza na magazeti yetu ya HabariLEO, Daily News, pia gazeti mtandao e-paper sambamba na video mtandao ya Daily News Digital na mitandao yetu ya kijamii,” amesema.
Mushi amesema TSN imeanza kuhudumu tangu miaka ya 1930 na wametunza kumbukumbu za kitambo chote hicho hivyo kujinasibu kuwa sehemu ya historia.