Watafiti wafundwa matumizi ya teknolojia

SERIKALI imewaasa watafiti, wabunifu na wagunduzi wa sekta mbalimbali nchini kuchukua hatua za makusudi katika kutumia teknolojia zinazoibukia ili kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini ikiwemo wabunifu wachanga kupata fursa za masoko.

Rai hiyo ilitolewa jijini Arusha na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa wakati alipofanya ziara ya siku moja kwaajili ya kutembelea vituo atamizi vilivyopo Arusha kwa lengo la kutambua na kuwezesha wabunifu kutoka kampuni changa kutumia teknolojia ili kufikia masoko.

Silaa amesema Rais Samia Hassan Suluhu anamaono ya kuwawezesha vijana wabunifu kutumia bunifu zao kwalengo la kuziatamia na kutafuta masoko kupitia teknolojia ya mawasiliano ili waweze kujikwamua kiuchumi kupitia bidhaa wanazozalisha kufikia masoko ya nchi za Jumuiya ya Afrika Masha riki(EAC) na nhi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC).

Amesema ni vema wabunifu, watafiti na wagunduzi kuchukua hatua ya kuchangamkia ajira kupitia sekta ya teknolojia ili kuuza bidhaa zao katika nchi za ndani na nje na kujikwamua kiuchumi.

“Serikali imetoa fursa mbalimbali katika bunifu ili kutatua changamoto za mambo madogo madogo wanazokutana nazo wabunifu lakini pia ni fursa ya kupata fedha na usaidizi ili wafikie malengo yao katika bunifu atamizi ili ndoto zao ziweze kuwa ajira “

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button