ARUSHA: Watafiti wa Masuala ya Sayansi wamesisitizwa kutumia takwimu sahihi za kitafiti zinazosaidia kugundua magonjwa ikiwemo utengenezaji wa dawa zinazosaidia kutibu magonjwa mbalimbali.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msoffe kwenye ufunguzi wa Mkutano wa nne wa Kimataifa wa Sterolojia unaofanyika Taasisi ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia (NM-IAST) kwakushirikiana na Chuo Kikuu Cha Ondohuz Mayis cha Uturuki ikishirikisha nchi 10 ikiwemo Tanzania.
Amesema tafiti hizo za kisayansi na teknolojia zinapotumiwa vema zinaweza kuondoa changamoto mbalimbali za magonjwa yanayoibuka ikiwemo kuyathibiti.
Naye Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) ,Profesa ,Maulilio Kipanyula mkutano huo unakutanisha wataalam hao kwa ajili ya kujengeana uwezo katika masuala ya sayansi , teknolojia na ubunifu kwa jamii hususan katika sekta ya afya .