Watajwa kuwa wasaidizi wa Trump

MAREKANI : RAIS Mteule wa Marekani,Donald Trump anatarajia kutimiza ahadi zake alizotoa kwa baadhi ya watu ambao amewaahidi kuwateua katika ngazi mbalimbali za uongozi kutokana na mchango mkubwa walioweza kuutoa katika kipindi cha kampeni.

Miongoni mwa watu hao waliopendekezwa ni Susie Wiles ambaye anatarajiwa kupewa nafasi kubwa katika jeshi la Marekani.

Wengine waliotajwa ni Brooke  Rollins, Robert F. Kennedy, Mike Pompeo hawa amepanga kuwapa nafasi ya uwaziri kama atapewa ridhaa na bunge la seneti kuwachagua.

Advertisement

Ric Grenell anaweza kupewa nafasi ya Mkuu wa Usalama wa Taifa nchini humo na Elon Musk yeye ameahidiwa  kuteuliwa kama kiongozi wa idara muhimu serikalini. SOMA : Trump kufutiwa mashtaka