Watakiwa kufanya ukaguzi kubaini mapungufu
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu ,Ridhiwani Kikwete amewaagiza maofisa kazi kufanya kaguzi za mara kwa mara kwenye maeneo ya kazi ikiwemo viwanda na migodi ili kubaini mapungufu yaliyopo na kuchua hatua stahiki.
Ridhiwani ametoa agizo hilo jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha Maofisa Kazi kutoka mikoa yote Tanzania Bara ,kilichoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
SOMA: WCF watakiwa kujiongeza
Amewataka maofisa hao kukagua maeneo ya viwanda na migodi kwani kumekuwa na malalamiko ya ukosefu wa vifaa vya kazi kwenye maeneo ya kazi na wengine wakifanya kazi kwenye mazingira magumu hususan kwenye viwanda hivyo wawekewe utaratibu wa kunywa maziwa baada ya kazi kutokana na mazingira halisi yaliyopo.
Amesema pia vibali vya kazi haswa baadhi ya maeneo hususan Mkoa wa Dar es Salaam kwani yapo malalamiko kuna watu wanaingizwa kinyemela bila kuwa na vibali vya kazi jambo hilo halikubaliki na wajue wanaikosesha serikali mapato lakini pia wanawanyima haki watanzania wenye sifa stahiki katika baadhi ya kazi.
“Mfano kunabaadhi ya maeneo nafasi ya ofisa rasilimali watu amejiriwa kutoka nje ya nchi na kazi ya HR ni kutambua watu anaofanya nao kazi sasa inakuwaje unakuwa na ofisa asiye mtanzania kwenye kazi ,hebu maofisa kazi timizeni makujumu yenu,nyie mwenzenu mimi hakuna mkubwa hapa zaidi ya Rais Samia Hassan Suluhu”
SOMA: WCF watakiwa kujiongeza