Watakiwa kushiriki miradi ya maendelo Mtwara

WANANCHI katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, wametakiwa kushiriki kikamilifu kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo inayowekezwa maeneo yao, ili kuharakisha maendeleo.

Rai hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas, wakati alipotembelea miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye Halmashauri hiyo na kupata fursa ya kuzungumza na wananchi wa maeneo mablimbali, ikiwemo wa Kijiji cha Miwindi kilichopo Kata ya Nanguruwe, wilayani humo.

Kijiji cha Miwindi ni eneo ambalo ujenzi wa shule ya sekondari unafanyika na unagharimu Sh Milioni 470 hadi kukamilika kwake na shule hiyo inatarajia kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2022/23.

Amesema kutokana na uchache wa fedha  zinazotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi kwenye maeneo yao, ni vyema wananchi washiriki kikamilifu katika ujenzi wa  miradi hiyo, kwani zipo kazi nyingi zinahitaji ushiriki wao

 

Habari Zifananazo

Back to top button