Watakiwa kusimamia wasanii mikoani kukuza sanaa

DAR ES SALAAM; MAOFISA Utamaduni nchini wametakiwa kuwajibika kikamilifu  kuwasimamia wasanii waliopo katika mikoa mbalimbali, ili kuhakikisha vipaji vyao vinatambulika na kustawi, badala ya kulazimika kuhamia Dar es Salaam kutafuta nafasi.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, alipokuwa akizungumza leo April 25,2025 katika kikao kazi cha maofisa utamaduni na maofisa maendeleo ya michezo kwenye ukumbi wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Amesema kuwa kuna wasanii wengi wenye vipaji vikubwa mikoani, hususa katika tasnia ya ucheshi, lakini wanakosa msaada na ufuatiliaji kutoka kwa maofisa utamaduni wa maeneo yao.

“Mikoani kuna wasanii wengi sana hasa wa comedy ambao hawapati nafasi ya kujitangaza wala kupata mikopo. Hawa wanatakiwa wasimamiwe na Maafisa Utamaduni, lakini kwa bahati mbaya hamuwasimamii,” amesema Msigwa.

Ameongeza kuwa ukosefu wa usimamizi wa karibu unasababisha wasanii hao wanapopata nafasi ya kuhamia Dar es Salaam wasiwe na hamu ya kurejea mikoani kwa kuwa hawakuwahi kupata sapoti kutoka kwa viongozi wa huko.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button