Watakiwa kutumia fursa za teknolojia kupata masoko

VIJANA nchini wametakiwa kutumia fursa za ukuaji wa teknolojia na matumizi ya kidigitali , ili kuweza kukuza ubunifu na ujasiriamali kupata masoko ndani na nje ya nchi.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Sahara Venture, Jumanne Mtambalike katika Kongamano la ubunifu, teknolojia na ujasiriamali lililoandaliwa Sahara Ventures kwa kushirikana na wadau wengine wakiwemi Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH).
“Tunafungua fursa mbalimbali kwa vijana kwenye maeneo ya ubunifu teknolojia pamoja na ujasiriamali, leo ni siku ya kwanza na tunafurahi tunategemea kuwa na wiki ambayo vijana watajifunza mambo mengi zaidi hadi Ijumaa, kuna matamasha na mada mbalimbali yatafanyika,”amesema.
Amebainisha kuwa wanashirikiana na COSTECH, kwa sababu wanawaunga mkono vijana katika kukuza ubunifu wao na wataendelea kufanya hivyo hata kwa vijana wa mikoani kufanya ubunifu na teknolojia kuendelea.
Mtabalike alisema wanatarajia vijana walioshiriki wapate mwamko kuanzisha biashara na kuendeleza ubunifu wao.