Watakiwa kuwekeza kilimo ch vanila

WANANCHI wa Mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kutambua faida zilizopo katika kilimo cha vanilla na kujikita kuwekeza katika kilimo cha vanilla, kutokana na tija ya kuwaendeleza kiuchumi, kwani  kina faida kubwa na kinastawi vizuri katika mkoa huo.

Hayo yamesemwa leo Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanila International Limited, Simon Mnkondya wakati akikagua mashamba yake ya vanila yaliyopo mkoani humo.

Amesema kilimo cha vanila kina tija kubwa ya kuwakwamua wananchi kiuchumi kama wataamua kuwekeza, kwani hakitumii muda mrefu kulima hadi kuvuna.

“Bado Watanzania wengi hawajafahamu siri hii ya kilimo cha vanila, lakini tunaendelea kutoa elimu wajue utajiri uliojificha katika uwekezaji huu wa vanila, kwani wale waliothubutu wameona faida zake, hivyo naendelea kuwahamasisha na kutoa elimu kwa kwa jamii juu ya kilimo hiki, wasipoteze muda kwa kuwekeza mazao yenye hasara,”amesema Mnkondya.

Akielezea mashamba yake, yaliyopo Mkoa wa Dar es Saam ameyataja kuwa ni Kunduchi na Ununio, Ubungo, Msewe na Boko Calfonia, ambapo vanila imestawi vizuri kwa zaidi ya mita 12 kwa rando(tawi), yanasababisha mkulima kupata fedha nyingi sana kwa maana marando ya vanilla ni biashara isiyokuwa na mipaka.

Pia amesema anao uwekezaji mkubwa uliopo katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Njombe, Dodoma, Kagera, Mwanza na mikoa mingineyo ambako anavuna utajiri wa fedha, hivyo wananchi wajitokeze kuwekeza kwa maendeleo yao.

Mkondya, ameishukuru serikali kwa kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji wa kilimo cha vanila nchini, jambo ambalo linafungua fursa zaidi kwa Watanzania wa ndani na nje ya nchi.

 

Habari Zifananazo

Back to top button