Watano mbaroni biashara ya upatu mitandaoni

JESHI la Polisi mkoani Mbeya, linawashikilia watuhumiwa watano akiwemo Meneja wa Kampuni ya LBL Gerald Masanya ,31, kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya upatu mtandaoni bila kuwa na kibali chochote ambapo ni kinyume na taratibu za kisheria.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Wilbert imeeleza baada ya kupata taarifa za uwepo wa Kampuni ya LBL Mbeya Media Limited kuwa inajihusisha na biashara ya upatu mtandaoni walianza kufuatilia kwa kushirikia na Maofisa kutoka Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mbeya na idara nyingine ambapo walifika maeneo ya Mwanjelwa na kuwakamata watumiwa hao.

Taarifa hiyo imewataja watuhumiwa hao ni Gerald Masanya ,31, ambaye ni Meneja wa Kampuni ya LBL – Mbeya, mkazi wa Nsalaga, Saphina Mwamwezi ,23, ambaye ni sekretari na mkazi wa Ituha, Edda William ,29, mkazi wa Uwanja wa Ndege wa Zamani, Yohana Mkinda ,29, mkazi wa Tukuyu pamoja na Macrine Sinkala ,23,.

Advertisement

Taarifa zinasema kuwa watuhumiwa kupitia kampuni hiyo wamekuwa wakijihusisha na biashara ya upatu mtandaoni na kueleza kuwa wamekuwa wakituma “link” maalum kwa wateja ili kujiunga mtandaoni na kisha wateja hutakiwa kulipa fedha kuanzia Sh 50,000 hadi Sh 540,000 na kutakiwa kuangalia matangazo ya “movies” mbalimbali zilizowekwa kwenye “Platform” hiyo kwa madai kwamba watapata faida baada ya kuwekeza fedha zao kwa kipindi fulani.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *