Dumisheni amani migogoro haina faida

TANGA : Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah amewataka watanzania kulinda na kuitunza amani ya nchi yetu ikiwemo kudhibiti viashiria vya uvunjifu wa amani pale vinapotokea.

Kauli hiyo ameitoa wakati akiongea katika mkutano maalum wa wajumbe wa CCM wilaya ya Kilindi ambapo amesema kuwa migogoro baina ya wakulima na wafugaji Kwa Sasa Haina tija kutokana na jitihada kubwa ambazo serikali imezifanya katika kumaliza changamoto zilizopo.

Amesema kuwa ni wakati Sasa umefika Kwa viongozi kuweza kusimamia maelekezo ya serikali ya kutoa elimu Kwa wananchi kuhusu namna bora ya kuishi Kwa upendo na kuvumilia baina yao.

“Mimi mlezi wenu nitafurahi kuona wananchi wanaishi Kwa maridhiano bila ya kugombani kwani wote ni watanzania na migogoro hiyo haina tija kwako Wala Kwa Taifa hili”amesema Makamu wa Rais.

SOMA : Tanzania yasisitiza umuhimu amani, usalama SADC

Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama hicho wilayani Kilindi Mkuu wa Wilaya Hashim Mgandilwa amesema tayari serikali imeshachukuwa hatua katika kumaliza mgogoro wa mipaka baina Kilindi na Kiteto.

“Tayari Mhe Rais Samia ametusaidia kumaliza changamoto hiyo Kwa kusaini  GN ya mipaka mpya hivyo niwaombe wananchi kuridhia na mabadiliko ambayo yameshafanyika Ili tuweze kuendelea kuishi kwa amani”amesema DC Mgandilwa.

Habari Zifananazo

Back to top button