Watanzania watano waula Stanbic Benki

DAR ES SALAAM: WATANZANIA watano huenda wakabadilisha mwelekeo wa maisha yao ikiwemo kujikwamua kiuchumi baada ya kila mmoja kushinda Sh 500,000 kutoka Benki ya Stanbic.

Ushindi wa kiasi hicho cha fedha umetokana na benki hiyo kuendesha droo ya pili ya mwezi kampeni ya Tap Kibingwa inayolenga kuchochea matumizi ya kadi za Visa Debit kwa ajili ya miamala ya kidijitali.

Kwa mujibu wa benki ya Stanbic washindi wa droo hiyo ya Machi ni Richard Muyambo, Alice Frank Mutagonda, Saddam Ally Nabbila, Abbasali Hirji na Siddharth Misra.

Aidha, Meneja wa kutoa kadi wa Benki ya Stanbic, Irene Mutahibirwa ameeleza kuwa dhamira ya benki hiyo ni kuendeleza malipo ya kidijitali nchini Tanzania kama moja ya njia za kuimarisha ubunifu wa kifedha nchini.

“Tap Kibingwa ni sehemu ya mkakati wetu mpana wa kuimarisha ubunifu wa kifedha na ujumuishi wa kifedha. Miamala ya kidijitali huleta usalama na ufanisi, na tunafurahia kuendelea kuwazawadia wateja wetu kwa kufanya maamuzi bora ya kifedha,” amesema Mutahibirwa.

Tap Kibingwa ni kampeni maalum inayoendeshwa na Benki ya Stanbic inayohamasisha wateja kutumia Kadi za Visa Debit kwa malipo ya kila siku badala ya pesa taslimu.

Kwa kuongezea amesema wateja wanaofanya miamala ya angalau shilingi milioni 5 kwa mwezi wanapata nafasi ya kushiriki kwenye droo za kila mwezi.

Kwa mujibu wa meneja huyo, kampeni hii inaendelea hadi mwisho wa Machi 2025, ambapo droo kubwa itamshuhudia mshindi mmoja akiibuka na gari jipya aina ya Suzuki Fronx 2024, zero mileage.

Kupitia Tap Kibingwa, Benki ya Stanbic inaendelea kudhihirisha dhamira yake ya kukuza ujumuishi wa kifedha na uvumbuzi wa kidijitali, kuhakikisha kuwa wateja wake wanapata huduma za benki zilizo salama, rahisi, na zenye manufaa.

Katika safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kidijitali, benki ya Stanbic inawahamasisha wateja wengi zaidi kutumia kadi zao kwa malipo na kujipatia fursa ya kushinda zawadi nono katika droo zijazo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button