WATU watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kwa tuhuma za mauaji ya wanandoa William Manyama na Christina Mahela, wakazi wa Kitongoji cha Mwagimagi, Kijiji cha Shilebela, Kata ya Ulewe, Halmashauri ya Ushetu.
Wanandoa hao wanakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 50-60, ambapo wamekatwa na kitu chenye ncha kali shingoni na maeneo mengine ya miili yao.
Kamanda wa Polisi mkoa, Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Juni 29 majira ya usiku wakiwa wamelala na tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina.
Amesema kulingana na upelelezi walioufanya hadi sasa wanawashikilia watu watatu na kwamba uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamni.
Kamanda Magomi amewaasa wananchi wasijichukulie sheria mkononi kwani kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Comments are closed.