Wateja 100 wa mwanzo kuunganishiwa maji Sh 50,000

WATEJA 100 watakaotangulia kuomba kuunganishiwa huduma ya majisafi kwenye mradi wa Ulemo – Misigiri, watatozwa bei ya promosheni ambayo ni Sh 50,000 tu.

Kaimu Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA), Mhandisi Richard Kasase, amekabidhi vifaa vilivyokamilika kuunganisha huduma kwa wateja hao, kwa uongozi wa Jumuiya ya Huduma ya Maji ngazi ya jamii, Kenkang’ombe, Kijiji cha Misigiri.

Kasase amesema vifaa hivyo vyenye thamani ya Sh milioni 35.62, vimepatikana kufuatia ahadi iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa SUWASA, Sebastian Warioba, wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea mradi huo Julai, mwaka jana.

Mradi wa Majisafi Ulemo-Misigiri, umetekelezwa na SUWASA kwa niaba ya Wizara ya Maji na kukamilishwa kwa gharama ya Sh milioni 669.3.

Habari Zifananazo

Back to top button