Watendaji watajwa kikwazo cha biashara

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo amesema juhudi za kuboresha mazingira ya biashara nchini Tanzania zinakabiliwa na changamoto kubwa ya kubadili mitazamo ya watendaji wa serikali.
Akizungumza jijini Dar es Salaam mbele ya Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, wakati wa mkutano wa uhakiki wa Mpango wa Pili wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (MKUMBI II), Prof. Mkumbo amesema kuwa licha ya viongozi wa juu kuwa mstari wa mbele katika kusukuma mageuzi, bado changamoto kubwa ipo katika utekelezaji katika ngazi za chini.
Ameeleza kuwa mashirika ya umma na mamlaka za udhibiti ndizo zenye jukumu kuu la kusimamia mazingira ya biashara, na iwapo hayatakuwa rafiki, taasisi hizo ndizo zitabeba dhamana ya hali hiyo.SOMA: Wafanyabiashara marufuku kupandisha mafuta
Kwa mujibu wa Waziri huyo, rasimu ya MKUMBI II imeainisha jumla ya changamoto 59 zinazokwamisha ufanyaji biashara Tanzania Bara na Zanzibar. Ili kukabiliana na changamoto hizo, mpango huo unapendekeza maeneo 11 ya kipaumbele yenye jumla ya hatua za mageuzi 246.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com