Watendaji wa halmashauri tekelezeni wajibu – Sawala

MTWARA: WATENDAJI wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara kila mmoja kwa nafasi yake ametakiwa kutekeleza wajibu wake ili halmashauri iendelee kuwa vizuri na mfano wa kuigwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Hayo yamejiri wakati wa kikao maalumu cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika kwenye halmashauri hiyo kuhusu kupitia na kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo halmashauri hiyo imepata hati safi ya CAG.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amesema ripoti inayotolewa CAG imekuwa ikisaidia kupima uwajibikaji, uadilifu, usimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa pia matumizi sahihi ya fedha.

Aidha ameutaka uongozi wa halmashauri hiyo kuwa, uhakikishe halmashauri inakuwa ya mfano ya kumaliza hoja za CAG ili waweze kuondokana na hoja zisizokuwa za lazima.

“Tumepokea taarifa ya CAG kwa ujumla tunaweza tukasema maeneo yote hayo inaonekana yamekwenda vizuri ndio maana hati iliyotolewa ni hati inayoridhisha”amesema Sawala

Kupitia ripoti iliyotolewa na Mkaguzi Mkuu wa nje wa Mkoa wa Mtwara Mwagwanga Peter amesema katika kipindi cha miaka mitatu 2021/2022 hadi 2023/2024 halmashauri ilikadiria kukusanya kukusanya Sh bilioni 9.2 na badala yake imekuanya Sh bilioni 10.8 hivyo kuvuka lengo la ukusanyaji kwa asilimia 118.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mtwara Vijijini Nashir Mfaume ameipongeza halmashauri hiyo kwa vile ambayo sasa imepiga hatua kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikilinganishwa na hapo awali.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button