Watoto 250 wakimbia ukeketaji

ZAIDI ya watoto 250 wanadaiwa kukimbia ukeketaji kila mwaka katika koo mbili kati ya 13 za Kikurya Wilaya za Serengeti, Butiama na Tarime mkoani Mara, hasa katika kipindi cha likizo za Desemba. Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Hope for Girls and Women Tanzania linalojihusisha na kupambana na ukatili wa kijinsia ndani ya jamii, Rhobi Samuel alisema kwa mwezi mmoja, watoto hao wamekuwa wakitoroka majumbani kwao na kukimbilia nyumba salama.
Rhobi alilieleza HabariLEO mjini Musoma kuwa, moja ya sababu zinazochochea ukeketaji ni baadhi ya wazazi kuwatambua mabinti wao kama chombo cha kifedha, huku wazee wa kimila wakitumia msimu wa likizo kuchagua mabinti kwa kupandisha dau zinazohusiana na michango ya kifedha kutoka kwa wazazi, kwa ajili ya sherehe za kijando. SOMA: Arusha, Manyara ukeketaji asilimia 43

Amesema licha ya jitihada za kutoa elimu, bado baadhi ya wazazi wameshindikana kuacha desturi hii, wakichukulia ukeketaji kama njia ya kupata mali au zawadi. Aidha, alidai viongozi katika baadhi ya maeneo wameonekana kuunga mkono vitendo hivyo, kwa kudai kuwa ni mila na desturi. Rhobi amezitaka jamii kwa ujumla kushirikiana na wadau na wanasiasa kutii sheria za nchi, kuheshimu haki za watoto wa kike na kutoa elimu badala ya kushikilia mila zinazokandamiza mabinti.
Shirika hilo limekuwa likijihusisha na utoaji wa elimu kwa ngazi za jamii kwa kukutana na wazazi, wazee wa kimila, viongozi wa vijiji pamoja na ngaliba ambao wamedaiwa kuwa kichocheo kikubwa cha vitendo hivyo. Rhobi alisema kwa msaada wa vipeperushi na majukwaa ya elimu, watoto wengi sasa wameanza kutambua hatari za ukeketaji na kujiweka salama wanapogundua hatari inavyowaelekea.




Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
.
More Details For Us →→ http://www.big.income9.com
Single Mom Reveals How She Earns $89k/Yr Working 10 Hrs/Week From Home. Tired of paycheck-to-paycheck living? Meet Kelly from New York—a regular mom who cracked the code to recession-proof income without selling a thing! Now,Big thanks …
.
Here is I started____________________ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com
https://www.bbc.com/swahili/medianuai/2012/11/121110_kisa_mkasa101112