watoto milioni 11 kupewa vitamini A

JUMLA ya vidonge vya matone ya vitamin A milioni 22 vyenye thahamani ya Sh bilioni 100.3 yamepokelewa na serikali kwaajili ya kuwapatia matone hayo watoto milioni 11 walio chini ya miaka mitano kwa kipindi cha mwaka mmoja ili kuwaongezea kinga mwili na kuimarisha afya ya macho kwa watoto hao.

Vidonge hivyo vilitolewa jijini Dare s Salaam na shirika la Nutritrion International na kukabidhiwa na Rais wa awamu ya nne ,Dk Jakaya Kikwete ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya menejimenti nchini wa shirika hilo.

Akizungumza wakati wa kutoa vidonge hivyo vya matone ya Vitamini A ,Dk Kikwete amesema matone hayo yatatolewa serikali ya Kanada ambapo yatatumika mara mbili kwa mwaka mmoja kwa mwezi Juni na Disemba.
“Faida ya vitamini hivi ni kuimarisha afya ya macho na kuongeza kinga ya mwili kwa mtoto hivyo ni muhimu kwa wazazi kuhakikisha watoto wanapatiwa matone haya,;alisema Dk Kikwete.

Advertisement

Akipokea matone hayo Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema Vidonge vya matone ya Vitamini A vitasaidia kuongeza kinga ya Mwili na kuimarisha afya ya macho kwa watoto walio na umri chini ya miaka tano.

Amesema elimu ya mtoto inaanza siku mimba inatunga na sio shuleni kwa kumpatia Mama lishe iliyobora wakati wa ujauzito ili kusaidia kuimarisha ubongo wa Mtoto.

“Wazazi zingatieni lishe bora kwa watoto tangu wa utangaji wa mimba na kuwa na desturi ya kula mlo bora kwa mama wajawazito na hii itamsaidia mtoto hata baada ya kuzaliwa na wakati yuko shule ubongo na akili yake kufanya kazi kikamilifu pia itamuepunga na magonjwa ya mara kwa mara” alieleza Dk Mollel.

Dk. Mollel amewataka watanzania kuzingatia milo yao ya kila siku kwa kupata chakula chenye lishe hasa vyenye vitamini ili kuepugana na magonjwa yasiyoambukiza kama shinikizo la damu , magonjwa ya moyo na kisukari
“hivi sasa watu wanakula kupitiliza na hawazingati chakula nyenye lishe ivyo na kupelekea watanzania kusumbuliwa na magonjwa yasiyoambukiza kama uzito uliopitiliza, shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na kisukari. Niwatake wahudumu wa afya ngazi ya jamii mkawape elimu watanzania waweze kutofautisha kati ya shibe na lishe.

/* */