TAASISI ya Doris Mollel Foundation imetoa msaada wa vitanda sita na mashine mbili za hewa ya oksijeni vyenye thamani ya shilingi milioni 13 katika hospitai ya rufaa Mkoa wa Mbeya.
Msaada huo ni kwa ajili ya kuwasaidia watoto njiti wanaozaliwa katika hospitali hiyo.
Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera ameipongeza taasisi hiyo kwa jitihada kubwa ambazo wamekuwa wakifanya kupambania maisha ya watoto njiti.
“Naipongeza Taasisi ya Doris Mollel kwa kuendeleza moyo wa kuwasaidia watanzania na wasio watanzania, niliwaona walipoenda Uganda kutoa msaada.” Amesema Homera
Aidha, Homera amewaomba watanzania na taasisi nyingine zaidi kujitokeza kuwasaidia watanzania wenzao bila mipaka.