TAARIFA kutoka Kusini mwa Taifa la Chad zinaeleza kuwa watu 10 wameuawa baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya wafugaji na wakulima. Gavana wa Mkoa wa Madoul, Adoum Forteye, ameeleza.
Taarifa ya Gavana Forteye ilieleza kuwa Alhamisi ya Mei 23, 2023 mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12 aliwapeleka wanyama kwa ajili ya malisho katika shamba la mkulima wa karanga hali iliyoibua ugomvi uliosababisha kifo cha kijana huyo.
Wazazi wa mtoto huyo waliwaua wakulima tisa kwa kulipiza kisasi, Amadou alisema, akiongeza kuwa tukio hilo lilitokea karibu na kijiji cha Bara II, kilomita 600 Kusini Mashariki mwa Mji Mkuu wa N’Djamena.
Imefahamika mara nyingi wakulima wamekuwa wakiwatuhumu wafugaji kwa kulisha mifugo mazao yao na kuyaharibu huku wafugaji wakisema kwamba wana haki ya asili ya kulisha mifugo kwenye maeneo hayo.
Machafuko ya aina hiyo yamekuwa yakiyatatiza maeneo yenye rutuba ya mpakani nchini Chad, Cameroon na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Hayo yanajiri wakati ambao maelfu ya wakimbizi wa Sudan ambao wengi wao ni wanawake na watoto wamekimbilia Chad tangu vita vianze katika nchi yao.
Taarifa zinasema katika wiki za hivi karibuni wakimbizi 90,000 wa Sudan wameingia nchini Chad