Watu 22 wapoteza maisha Beirut

LEBANON : MASHAMBULIZI  ya Israel katika eneo la katikati mwa mji mkuu wa Lebanon, Beirut yamewauwa watu 22, wengine wamejeruhiwa na kusababisha uharibifu mkubwa.

Mashambulizi hayo ya anga yameporomosha jengo moja la ghorofa nane na jengo jingine kuharibiwa vibaya.

Kituo cha Televisheni kinachoendeshwa na kundi la Hezbollah, cha Al Manar kimeripoti kwamba jaribio la kumuua afisa mwandamizi wa shughuli za usalama wa kundi hilo Wafiq Wafa halikufanikiwa.

Advertisement

Kituo hicho kimesema Wafa hakuwemo kwenye majengo yaliyoshambuliwa na Israel.

Mashambulio ya Israel dhidi ya maeneo yanayokaliwa na wakaazi kusini mwa mji mkuu Beirut yameongezeka.

Kundi la Hezbollah linaendesha operesheni zake nyingine kwenye eneo hilo la Kusini.

SOMA : Israel yashambulia ngome za Hezbollah