Watu 80000 wamekimbia makazi DRC

DR CONGO: SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi (UNHCR) limesema watu  elfu themanini wamekimbilia nchi jirani kufuatia mzozo unaoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Takriban watu 61,000 kati ya hao wamekimbilia Burundi kuomba hifadhi, nchi ambayo imepokea idadi kubwa ya wakimbizi kutokana na mapigano kati ya vikosi vya serikali ya DRC na kundi la waasi la M23.

Uungwaji mkono wa Rwanda kwa kundi la M23 umewezesha waasi hao kuchukua udhibiti wa maeneo mengi ya mashariki mwa DRC, yenye utajiri wa madini, na kusababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao.

Hali hii imepelekea kile ambacho UNHCR imekitaja kama moja ya majanga mabaya zaidi ya kibinadamu duniani. SOMA: Wakazi laki moja wakimbia makazi Congo

Ujerumani imesema itasitisha msaada mpya kwa Rwanda kutokana na mashambulizi ya kundi la M23 mashariki mwa nchi hiyo, ambapo kwa mujibu wa watalaamu wa Umoja wa Mataifa, waasi hao wanasaidiwa na wanajeshi wa Rwanda.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button