Watu kumi wauawa kwa risasi Sweden

SWEDEN : TAKRIBAN watu 10 wameuawa kwa risasi katika shambulio lililotokea katika Kituo cha Elimu cha Risbergska kilichopo katikati mwa Sweden.
Mkuu wa Polisi wa Sweden, Roberto Eid Forest, alieleza kuwa shambulio hili linachukuliwa kama moja ya mashambulizi mabaya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo.
Forest aliongeza kuwa idadi kamili ya majeruhi bado haijulikani kutokana na idadi kubwa ya watu walioathirika. SOMA: Watu wanne wapigwa risasi Georgia
Hata hivyo, Polisi hawajatoa taarifa rasmi kuhusu kama waliopoteza maisha ni walimu au wanafunzi.”Mtuhumiwa huyu bado hajulikani na polisi na hana uhusiano na kundi lolote la kihalifu,” Forest alisema.
Aliendelea kusema: “Hatutaraji kutokea kwa mashambulizi mengine ya risasi katika siku zijazo,” akiongeza matumaini ya kuepusha mashambulizi zaidi.
Katika miaka ya hivi karibuni, Sweden imeshuhudia ongezeko la mashambulizi ya risasi na mabomu, jambo ambalo limeleta wasiwasi mkubwa kwa wananchi wa nchi hiyo.



