Watu wanne wapigwa risasi Georgia
MAREKANI : WATU wanne wameuawa baada ya mwanafunzi mwenye umri wa miaka 14 kufyatua risasi katika shule ya sekondari huko Gerogia nchini Marekani.
Taarifa zinasema kuwa waliouawa wametambulika kuwa ni wanafunzi wawili na walimu wawili.
Tukio hili la mauaji liliwafanya wanafunzi na watu wengine waliokuwa katika eneo hilo kukimbia katika maeneo mbalimbali kujificha.
Taarifa za polisi nchini Marekani zinasema kuwa watu wote wanne waliouawa wameweza kutambulika huku majeruhi wengine wakikimbizwa hospitalini .
SOMA : Marekani yasitisha msaada wa silaha Israel
OMA : Hatahivyo mwanafunzi aliyefanya shambulio hilo la mauaji amejisalimisha katika vyombo vya sheria baada ya kufanya mauaji hayo.
SOMA : Kijana mmoja amewafyatulia risasi wanafunzi na kuua mmoja na kuwajeruhi wengine nchini Marekani