Watu Tisa wapoteza maisha Lebanon

LEBANON : WATU wasiopungua tisa wameuawa na maelfu kujeruhiwa baada ya mamia ya vifaa vya mawasiliano ulipuka nchini Lebanon.

Waziri wa Afya Firas Fabias amesema watu wasiopungua 2,750 wamejeruhiwa na zaidi ya 200 wana hali mbaya kwenye maeneo kadhaa ya Lebanon na hasa yanayodhibitiwa na wanamgambo wa Hezbollah

Kundi hilo limesema wapiganaji wake wawili pia wameuawa na wengine wamejeruhiwa nchini Syria ambako pia kumetokea milipuko.

Advertisement

Umoja wa Mataifa umeendelea kuonya kuhusu mzozo  unaoendelea kati ya Lebanon na Israel ambao unachangia kuongeza hali ya wasiwasi  nchini humo.

SOMAMarekani yasitisha msaada wa silaha Israel