WANATASNIA ya habari wameagizwa kuzingatia kanuni, maudhui na maadili ya uandishi wa habari ikiwemo kupeuka watu wasio na elimu wala ujuzi “vibaka” kujikita wanahabari.
Hayo yamesemwa na mkongwe wa habari, Betty Mkwasa ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Maudhui kutoka Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA) wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya utangazaji.
Mkwasa amesema kuna watu wasio na elimu ya uandishi wa habari wameingilia tansia ya habari na kutangaza maudhui yao binafsi bila kuweka mizani husika kwa kuwataja watu bila kiwatafuta ili mradi wapate wasomaji au wafuatiliaji wengi katika habari zao kwenye vyombo vyao husika.
SOMA:Waandishi wa habari wafundwa
“Lazima tuzingatie maadili ikiwemo mavazi yetu lakini pia tufiche watu tunaowahoji haswa matukio ya ubakaji ulawiti na mengineyo,nasisitiza kuzangatia maadili ya taaluma zetu”