Watu zaidi ya 50 wauawa DR Congo

CONGO: WATU zaidi ya 50 wameuawa na wapiganaji wa kundi la waasi la Codeco Militia katika Kijiji cha Djaiba kilichopo katika Jimbo la Ituri Kaskazini Mashariki mwa Jamjuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Taarifa hiyo imetolewa na Shirika la Habari la Reuters, ambapo amesema kwa mujibu wa vyanzo vya serikali ya kijiji hicho, wapiganaji wa kundi hilo zaidi ya 120 walivamia na kuanza kuwarushia risasi raia waliokuwa katika kijiji hicho ambacho kinasifika kwa kuwa na utajiri wa migodi ya madini.

Kiongozi wa kijiji hicho, Antoinnette Nzale amesema kijiji hicho mbali na kuwa na utajiri wa madini, pia kinatumika kama sehemu ya makazi kwa wananchi waliokimbia mapigano maeneo mengine ya Jimbo la Kivu Kaskazini na Jimbo la Ituri nchini humo.

Advertisement

Nzale amesema watu 55 wameuawa papohapo huku akidokeza kuwa huenda vifo vikaongezeka kwa kile alichodai bado shughuli ya kuwatambua waliouawa na waliojeruhiwa inaendelea.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *