Watuhumiwa nyara za serikali wakamatwa

JESHI la polisi mkoani Kagera linawashikilia watu watano kutoka sehemu tofauti Tuhuma za kukutwa na nyara za serikali.
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera ,Brasius Chatanda aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Fidelis Ikanga (35) mkazi wa Kagenyi wilaya ya Karagwe,Giburiru Dauda (58) mkazi wa wilaya ya Missenyi, Jeofrey Malingumu (35) mkulima mkazi wa Wilaya Missenyi ,Sulaiman Semukuye 57 Raia wa Uganda ,Idephonce Karongo 58 mkulima mkazi wa wilaya ya Kyerwa.
Amesema Februari 24 mwaka 2025 katika Wilaya ya Karagwe watuhumiwa wawili walikamatwa wakiwa na pembe mbili za mnyama aina ya Faru baada ya kuwekewa mitego kadhaa na kuikwepwa na baada ya hapo wakawekewa mtego wa Sh milioni 250.
Jeshi la polisi mkoani humo linaendelea kubaini mtandao mzima unahojihusisha na uporaji wa nyara za serikali pamoja na mazao ya misutu.
Aidha jeshi hilo linaendelea kufatilia kwa ukaribu mauaji ya Francis Butoto ambayo yalitokea Februari 22, 2025 kijiji ccha kishanda kata kibare tarafa ya Murongo wilayani Kyerwa ambapo watuhumiwa wanne wamekamatwa
Walikamatwa ni Frola Bitakamile(42)ambaye ni mke wa Marehemu,George Bitaka (52) Derrick George (19) Christopher Bitakamile (30)
Alisema baada ya watu hao kufanya mauaji wananchi wenye hasira kali walichukua sheria mkononi na kwenda kuharibu mali za Bitakalamile na wanaye wanne kwa kufyeka shamba ekari 10 mibuni hekari 1 ,kuchoma moto nyumba ,kuchoma moto magari mawili na pikipiki tano.
Jeshi la polisi linaendelea kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za uharibifu na uhalifu na kucha kujichukulia Sheria mkononi.



