Wawili mbaroni lita 2,120 mafuta ya SGR

JESHI la Polisi mkoani Tabora limewakamata watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na lita 2,120 za mafuta ya dizeli yanayodaiwa kuibwa katika kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga reli ya kisasa (SGR) kipande cha kutoka Tabora hadi Makutopora.

Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Richard Abwao alisema watuhumiwa walikamatwa Aprili 2 saa 4.30 usiku.

Kamanda Abwao alisema mafuta hayo yalikamatwa kutokana na kazi iliyofanywa na walinzi na Jeshi la Polisi Wilaya ya Tabora ambao walikamata gari aina ya Suzuki lenye namba za usajili T 841 AUJ likiwa na madumu 53 ya mafuta ya dizeli.

Alisema pia walikamata pikipiki aina Sanlg yenye namba za usajili MC 861 AHC iliyokuwa ikitumiwa na watuhumiwa katika wizi huo. Wakati huohuo katika doria inayoendelea katika Wilaya ya Tabora mjini polisi walikamata mtu akiwa na viuawadudu aina ya EAKILI135C chupa 178 na SETECRON PLUS 440EC chupa 87 ambavyo ni mali ya serikali.

Kamanda Abwao alisema viuatilifu hivyo vipo chini ya Bodi ya Pamba Tanzania na mtuhumiwa hakustahili kuwa navyo kwa kuwa hakuwa na vibali halali vya ununuzi wa bidhaa hizo.

Habari Zifananazo

Back to top button