Wazawa waomba ulinzi dhidi ya wawekezaji

DAR-ES-SALAAM : JUMUIYA ya wafanyabiashara wa soko la Kariakoo, chini ya Mwenyekiti wao Severin Mushi, imeiomba serikali kuchukua hatua madhubuti ili kuwalinda wafanyabiashara wazawa dhidi ya uvamizi wa wawekezaji wa kigeni wanaoendesha biashara ndogondogo katika eneo hilo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mushi amesema kuna umuhimu wa serikali kuboresha usimamizi wa sheria, kuimarisha elimu ya kodi, na kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara wazawa ili kuleta maendeleo ya kiuchumi nchini.

“Kwa sasa, wafanyabiashara wazawa wameiomba serikali kuingilia kati kwa kuwaingilia wafanyabiashara wageni wanaokuja kama wawekezaji, lakini wanashiriki kwenye biashara za kawaida kama wachuuzi,” amesema Mushi.

SOMA: Tuzo za wafanyabishara Kariakoo zaja

Kwa upande wake, Katibu wa wafanyabiashara wa Kariakoo, Renatus Mlelwa, amesisitiza kwamba wawekezaji wa kigeni wanapaswa kujikita zaidi kwenye sekta ya viwanda na uzalishaji, badala ya kuingilia biashara za rejreja na kuzuia nafasi za wafanyabiashara wazawa.

“Changamoto kubwa ni wafanyabiashara wageni wanavyowasumbua walju yao. Tunaomba serikali kuweka utaratibu mzuri kati ya BRELA, Uhamiaji, na Wakala wa Ajira ili kufanya tofauti kati ya mfanyabiashara na muwekezaji,” amesema Mlelwa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button