Wazazi CCM Dar sasa kamili

JUMUIYA ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam hatimaye imepata safu mpya ya viongozi wake baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Khadija Ally kuitisha Baraza rasmi na kuteua wajumbe wa baraza hilo na wajumbe wa kamati ya utekelezaji kwa ridhaa wajumbe wa Baraza la Mkoa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kukamilisha kuipata safu ya wajumbe wake Khadija amesema, baada ya safu ya uongozi wa Jumuiya hiyo kukamilika sasa wanaelekeza nguvu kwenye mambo matano.

“Kwa sasa safu ya Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam imekamilika ambapo ina wajumbe wa kamati ya utekelezaji,  wajumbe wa kamati tendaji lakini pia wajumbe wa baraza rasmi.” Amesema Khadija na kuongeza

“Sasa naomba nitoe dira kuwa Mkoa wa Dar es Salaam Jumuiya ya Wazazi inakwenda kusimamia mambo yake makuu matano ambayo ni elimu, malezi, afya, mazingira na uchumi katika Mkoa wa Dar es Salaam.

“Jumuiya ya Wazazi CCM inadili na mambo hayo matano na kama mnajua Mkoa wa Dar es Salaam mmomonyoko wa maadili umekithiri sana hivyo tunakwenda kudili na hilo na hayo mengineyo.

“Jumuiya kwa kushirikia na makatibu wetu wa kata zetu zote 102 tutahakikisha tunatoa mafunzo ya uongozi kupitia kamati za utekelezaji na kamati za wilaya.

Amesema Jumuiya ya Wazazi inakwenda kuandaa mpango kazi wa miaka mitano kuhakikisha majukumu yake hayo yanafanyika kifasaha na kurejesha heshima na hadhi ya jumuiya  na kufanyakazi iliyotukuka kuhakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi Mkuu wa 24/25.

 

Habari Zifananazo

Back to top button