Wazazi pelekeni watoto vituo vya malezi
SONGWE: WAZAZI na walezi mkoani Songwe wametakiwa kuwapeleka watoto wadogo wenye umri kuanzia miezi 18 mpaka miaka minne katika vituo vilivyosajiliwa vya malezi ,makuzi na maendeleo ya awali kabla hawajaanza elimu ya awali ili kupata malezi yenye mwitikio na kugundua vipaji vyao .
Hayo yamezungumzwa na Isdory Ntara Msimamizi wa Asasi ya Health & insurance management services organization (HIMSO) ambayo ni kinara Mkoa wa Songwe katika kutekeleza programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto (PJT-MMMAM).
Akizungumza katika Uzinduzi wa wa Kituo Cha Tegete Kid’s Day Care kinachohusika na malezi Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto katika mji wa Mlowo Wilaya ya Mbozi, amesema “ubize” wa wazazi na walezi katika shughuli mbalimbali huathiri makuzi yenye mwitikio kwa watoto.
“Umri wa miaka sifuri mpaka miaka nane ndio umri sahihi wa kumpatia malezi bora mtoto yanayoendana na maadili mema, elimu na kufundishwa kufanya kazi tangia wakiwa wadogo,
Hivyo ni vema kupelekwa kwenye vituo vya malezi ambavyo watoto hupata nafasi ya kuchangamana na wenzao na kupata malezi bora kutoka kwa walimu wenye taaluma ya Malezi” amesema Ntara