Wazazi watakiwa kuacha kuwaonesha watoto katuni

WAZAZI na walezi wametakiwa kuacha tabia ya kuwaachia watoto kuangalia katuni zisizo na maadili badala waongee nao ili kubaini changamoto wanazokumbana nazo mashuleni, majumbani na mitaani ili kudhibiti matukio ya ukatili.

Akizungumza na wanawake wa Jiji la Arusha katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, yenye  Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mutahengerwa amesema endapo mzazi atabaini  chaneli zinaviashiria vya ushoga au udhalilishaji wachukue hatua ili kudhibiti matukio ya ukatili.

“Vitendo vya ukatikili wa jinsia bado zinaendelea haswa kwa wanawake na watoto ikiwemo watoto wa kiume ambao bado wanasahaulika ingawa nao wanafanyiwa ukatili wa aina mbalimbali.”amesema

Takwimu zinaonesha kwa mwaka2022 vitendo vya ukatili wa kijinsia vilivyoripotiwa 8,647, ukatili wa kisaikolojia 12,515 huku ukatili wa kingono 5,781.

Ofisa Maendeleo ya  Jamii Mkoa wa Arusha, Blandina Nkini aliishukuru serikali kwakutoa mikopo ya sh,1,390,193,600 kwa mwaka wa fedha 2022/23 ambapo vikundi vya Wanawake 121,vijana 42 na watu wenye ulemavu2

Habari Zifananazo

Back to top button