Wazee Simanjiro wamkarimu Chongolo, alala kwenye boma

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amehitimisha ziara yake wilayani Simanjiro kwa kuzungumza na wenyeviti wa mashina yote ya Kata ya Orkesumeti kisha wakamuomba alale kwenye moja ya boma la viongozi hao,ombi aliloridhia.

Chongolo alitii ombo hilo la wazee jana usiku katika Shina nambna 35 Tawi la Njiro katika kata hiyo wilayani hapa mkoani Manyara kwa kushiriki nao chakula cha jioni, kisha kulala katika boma la jamii ya wafugaji.
Awali Chongolo akiwa wilayani humo alikagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM 2020/25,uhai wa chama mashinani na kuzungumza na makundi ya jamii.

Chongolo ameambatana na wajumbe wawili wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Sophia Mjema na Katibu wa NEC Oganaizesheni, Issa Gavu.
Leo kiongozi huyo ameanza ziara wilayani Kiteto na atakagua utekelezaji wa ilani kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo na kukagua uhai wa chama mashinani na kusikiliza kero na changamoto za makundi mbalimbali.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button