Wazee, yatima wapewa zawadi ya Idd Tanga

WAZEE pamoja na watoto yatima wanaoishi katika mazingira magumu waliopo mkoani Tanga wamepatiwa zawadi kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Idd el Fitr na Rais Samia Suluhu Hassan.

Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Rais Samia,  Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amesema kuwa zina lengo la kuonesha upendo na moyo wa kujali alionao Rais Samia.

“Rais wetu anajua kwamba kesho waislamu wanasherehekea sikukuu ya Eid baada ya kumaliza Mfungo wa Ramadhani, hivyo ameonea ni vyema kuyakumbuka makundi hayo muhimu, ili nao waweze kufurahia sikukuu kama wengine,”amesema RC Kindamba.

Vituo viwili vya kulelea watoto yatima pamoja na makazi ya wazee ya Mwanzange yaliyopo jijini Tanga, vimepatiwa zawadi za chakula Kwa ajili ya kusherehekea sikukuu hiyo.

Habari Zifananazo

Back to top button