Waziri Aweso atumia bodaboda kukagua mradi wa maji

WAZIRI wa Maji , Jumaa Aweso ametumia usafiri wa pikipiki (bodaboda), kutembelea na kukagua mradi mkubwa maji wa Morong’anya uliopo Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, wilaya ya Morogoro.

Aweso amelazimika kutumia usafiri hiyo kutokana na changamoto ya barabara kuelekea kwenye mradi na chanzo cha maji kutofikika kwa njia ya gari.

Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Sospeter Lutonja, amesema mradi huo unaotekelezwa katika Jimbo hilo unagharimu zaidi ya Sh bilioni 23, ambazo zimetolewa na serikali.

Amesema mradi huo utakapokamilika utahudumia wananchi zaidi ya 52,000 wanaishi kwenye vijiji 19 katika kata saba za jimbo hilo.

Waziri Aweso pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo , Hamisi Shabani Taletale “ Babu Tale” na watendaji wengine wa serikali, mamlaka za maji na wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wamelazimika kuacha magari yao na kutumia usafiri wa bodaboda, ili kulifikia eneo la mradi huo.

Baada ya kufika eneo la mradi Waziri Aweso alishiriki upandaji miti kando ya chanzo cha maji katika mto Mbezi ambao unatumika kama chanzo kikuu cha maji kwa mradi huo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button