Waziri Biteko awapa somo wachimbaji wadogo

WAZIRI wa Madini, Dk Dotto Biteko, ametoa angalizo kwa wachimbaji wadogo wa madini kutotumia vibaya uhuru wa kuendesha shughuli zao waliopewa na serikali, bali wanapaswa kuheshimu wawekezaji na sheria za nchi.

Dk Biteko amesema hayo Januari 3, 2022 alipotembelea mgodi wa Isonda uliopo kijiji cha Isonda, wilayani Nyang’hwale mkoani Geita kusuluhisha taharuki iliyoibuka kati ya wachimbaji wadogo na mwekezaji kutoka China.

Amebainisha taratibu za uchimbaji zinaelekeza mmiliki wa leseni kuheshimiwa, hivyo wachimbaji wadogo wanapaswa kuzingatia hilo na kuacha kujiona wao ndiyo wenye haki zaidi ya wawekezaji.

Advertisement

Amekemea wachimbaji wadogo wa Isonda kuendekeza ubaguzi kwa mwekezaji, kampuni ya Henan Mining, ambao ni wamiliki halali wa leseni za eneo hilo lenye ukubwa wa kilomita za mraba nane.

“Sasa kama hali ni hiyo, mwenye leseni ana wajibu wa kulinda leseni yake, na sisi tuna wajibu wa kutokuvamia leseni ya mtu mwingine,” ameelekeza na kuongeza:

“Huyu mnayemuita mwekezaji, abaki kwenye eno lake, lakini kwa sababu hapa kuna wachimbaji wadogo, nao waendelee na shughuli zao, wachimbe nao wajitibu na shida zao.

“Pili msimgeuze huyo mwekezaji kuwa adui, mkimgeuza kuwa adui, sheria zipo, zitakuja hapa zitaelekeza utaratibu, kwani na nyie hapa siyo kwamba mpo hapa ndio mna haki zaidi.”

Dk Biteko ameelekeza Ofisi ya Madini, Mkoa wa kimadini Mbogwe kuweka utaratibu utakaowafanya wachimbaji wadogo kuendelea na shughuli zao kwenye hekta 20 na eneo linalobaki aachiwe mwekezaji.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *