Waziri Kairuki akutana na Rais wa Utalii Duniani

SAUDIA ARABIA; Riyadh. Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki amekutana na kufanya mazungumzo na Rais ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Utalii Duniani (World Travel Tourism Council (WTTC) , Bi. Julia Simpson kwa lengo la kujadili namna bora ya kushirikiana katika kutangaza na kukuza utalii endelevu nchini Tanzania.
Kikao hicho kilifanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Four Seasons jijini Riyadh, Saudi Arabia.
Tanzania ikiwa mwanachama wa WTTC itaendelea kujitangaza Kimataifa na itapata fursa ya kuwa mjumbe katika nafasi mbalimbali.
Baraza hilo lina mtandao wa mashirika binafsi zaidi ya 200 Duniani wanaotoa huduma mbalimbalia zenye lengo la kukuza utalii.
Aidha, katika kuendelea kutangaza utalii na kutafuta masoko mapya ya utalii, Waziri Kairuki amefanya mazungumzo na wadau wakubwa wa utalii duniani ikiwa ni pamoja na Meneja Masoko wa Shirika la Ndege la Saudi Arabia, Abdulrahman Alabdulwahab kwa lengo la kuangalia namna bora ya kuitangaza Tanzania kupitia ndege za shirika hilo na kushirikiana katika kutangaza vivutio vya Utalii nchini.
Pia, amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa City Sightseeing World wide, Enrique Ybarra kwa lengo la kuangalia namna bora ya kuweka matangazo ya vivutio vya Tanzania kwenye vyombo vyake vya usafiri, na katika tovuti maarufu duniani ijulikanayo kama Isango.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
money
money
2 months ago

Mashindano ya nani kuhinda kwenye neno “ABROAD“ NCHINI TANZANIA!?

MJERUMANI

MHINDI

MTANZANIA

MKENYA

MNIGERIA

MHISPANIA

file:///C:/Users/User/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image002.jpg

NANI AINGIZE NDEGE ZA KWENDA KUMSALIMIA BABU NA BIBI, KWA ALIYESHINDA KULELEWA NA BIBI TU!?

Capture.JPG
money
money
2 months ago

Mashindano ya nani kuhinda kwenye neno “ABROAD“ NCHINI TANZANIA!?

MJERUMANI

MHINDI

MTANZANIA

MKENYA

MNIGERIA

MHISPANIA

file:///C:/Users/User/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image002.jpg

NANI AINGIZE NDEGE ZA KWENDA KUMSALIMIA BABU NA BIBI, KWA ALIYESHINDA KULELEWA NA BIBI TU!?..

Capture1.JPG
Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x