Mashindano gofu hifadhi ya Serengeti yameiva

MARA; Wachezaji 81 kutoka nchi  za  Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Malawi wanatarajiwa kushiriki mashindano ya gofu yanayoanza  Alhamisi ya Octoba 15, 2026.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 14, katika eneo la Fort ikoma pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa  Serengeti, Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Massana  Mwishawa, amesema mradi wa ujenzi wa uwanja wa gofu ulizinduliwa rasmi Desemba 29, 2022, na Bodi ya Wadhamini ya TANAPA, iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali George Waitara.

Amesema tayari Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limekamilisha ujenzi wa uwanja huo na kwamba Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji, anatarajiwa kuuzindua  Oktoba 18, 2026, ambayo takuwa pia siku ya mwisho ya mashindano hayo.

Ameeleza uwekezaji huo unaakisi dhamira ya TANAPA ya kuendeleza bidhaa bunifu za utalii zinazokamilisha uzoefu wa kutembelea vivutio vya wanyamapori, kuhamasisha watalii kukaa kwa muda mrefu zaidi na kuongeza thamani ya kiuchumi ya vivutio vya asili vya Tanzania.

Mwishawa amefafanua kuwa  uwanja huo upo Fort Ikoma, pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, na umejengwa, ili kuwapa watalii wanaotembelea eneo hilo fursa ya kushiriki shughuli nyingine za burudani, ikiwemo mchezo wa gofu.

Ameeleza  baada ya uzinduzi, uwanja huo utaendelea kuwa miongoni mwa shughuli za utalii zitakazopatikana kwa wageni wanaotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na maeneo ya karibu, kwa kuwapa huduma za ziada na uzoefu tofauti wanapokuwa nchini.

Amefafanua kuwa miundombinu iliyokamilishwa inajumuisha maeneo ya kuchezea na kufanyia mazoezi, jengo la huduma kwa wachezaji, barabara, mifumo ya maji na umeme, miundombinu ya umwagiliaji pamoja na mabwawa ya kuhifadhi maji.

Mwishawa amesema uwanja huo ni sehemu ya juhudi za TANAPA za kuendeleza bidhaa mpya za utalii, kuongeza thamani ya vivutio vya hifadhi za taifa na kuimarisha nafasi ya Tanzania katika masoko ya kimataifa ya utalii.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills. This is what I do….. https://www.work27.info

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button