Waziri Mchengerwa ataka tathmini kuvurunda Stars

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa, amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kukutana mara  moja na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), pamoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), ili kujadili mwenendo wa Taifa Stars.

Taarifa iliyotolewa leo na  Mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini, John Mapelele, mbali na suala hilo Waziri Mchengerwa, ameagiza pia kupitia kikao hicho waandae mkakati kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri.

Jumamosi iliyopita timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, ilifungwa mabao 3-0 na Uganda ‘The Cranes’ mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN).

Mchezo huo uliofanyika Uwanja wa St Mary’s Kitende, mjini Entebbe, nchini Uganda umeifanya Taifa Stars kutolewa kwa jumla ya mabao 4-0, baada ya mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Stars kulala bao 0-1.

Habari Zifananazo

Back to top button