Waziri Mkuu aridhishwa maandalizi Mei mosi

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maandalizi kuelekea sherehe za siku ya wafanyakazi duniani zitakazofanyika kesho Mei 1, 2023 kitaifa mkoani Morogoro katika Uwanja wa Jamhuri.

Ameyasema hayo leo Jumapili (Aprili 30, 2023)alipopokea taarifa na kukagua maandalizi ya maadhimisho ya sherehe hizo. ambazo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Majaliwa ameipongeza kamati inayoratibu sherehe hizo na kuwataka kuhakikisha wanakamilisha maeneo ambayo yanahitaji maboresho.

Advertisement

Awali, akitoa taarifa ya maandalizi hayo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi   Fatuma Mwasa amesema maandalizi yamekamilika kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, Tumaini Nyamhokya amesema kwa upande wa vyama vya wafanyakazi maandalizi yamekamilika na wanamatarajio kuwa mahudhurio yatakuwa makubwa na sherehe hizo kuwa za mafanikio.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *