Waziri Mkuu: Miradi 215 kutoa ajira 13,000

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi jumla ya miradi 215 imesajiliwa kupitia Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) yenye thamani ya Dola bilioni 3.26.

Akizungumza leo Jaruari 11, 2023 mara baada ya kuzindua mradi wa hoteli ya Kilindini ikiwa ni sehemu ya matukio muhimu yaliyojumuishwa katika maadhimisho ya sherehe za miaka 59 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, Waziri Majaliwa amesema miradi hiyo inatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 13,000.

“Mafanikio haya yote kwa kipindi hiki kifupi, yamechangiwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Nane zikiwemo sera na mipango madhubuti iliyowekwa na Chama cha Mapinduzi kupitia Ilani yake ya Uchaguzi ya Mwaka 2020.” amesema Waziri Mkuu.

Amesema wananchi wanapaswa kuyaenzi mapinduzi hayo kwa sababu ndicho chombo kilichowavusha kutoka katika gharika za kutawaliwa na kubaguliwa katika nchi yao.

“Kwa mnasaba huo, sherehe hizi za kuadhimisha Mapinduzi matukufu ya Zanzibar zinakua ni sehemu ya historia muhimu kwani zinatukumbusha jinsi ambavyo wakulima na wafanyakazi wanyonge walivyokataa madhila ya kubaguliwa na kunyanyaswa.” ameongeza Waziri Majaliwa.

Amesema kuwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan na Rais Dk Mwinyi wanao mkakati endelevu wa kukuza sekta ya uwekezaji nchini ikiwemo kushirikisha sekta binafsi nchini na kuvutia mitaji kutoka nje kwa lengo kuhakikisha nchi zetu zinakuwa na uchumi imara

Habari Zifananazo

Back to top button