Wema ataka wasanii warudi shule

DAR ES SALAAM; Mwigizaji na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu amesema kuna haja ya wasanii kurudi shuleni, ili kuongeza ujuzi na maarifa yatakayowasaidia kuboresha kazi zao za filamu.

Pia amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufikiria kufanya mabadiliko makubwa katika sekta hiyo na kuwapa nafasi wasanii kwenda kwenye mafunzo na kuahidi hawatamuangusha.

Katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuzungumzia safari yao ya Korea Kusini, Wema amesema suala la elimu linahitajika kwa watu wote wanaohusika kwenye uigizaji kwa kuwa itawasaidia kufanya kazi kitaalamu na sio kubahatisha.

“Watu wasifanye kazi kwa uzoefu tunahitajika kurudi shule namaanisha wasanii, wahariri, waandishi wa hadithi, waongozaji, naamini kuna kozi mbalimbali zinaweza kutusaidia na Mama atatusaidia,”amesema.

SOMA: Monalisa: Safari yangu Korea imekuwa ya ajabu

Kauli hiyo inakuja baada ya kundi la pili la wasanii kutoka Korea Kusini kwenye mafunzo na kujionea namna wenzao wamepiga hatua kubwa, akisema hata wao wanayo nafasi ya kubadilika kutokana na kile walichojifunza.

Mbali na hilo, amesema wanahitaji kupata eneo kubwa lisilopungua ekari 200 kwa ajili ya kufanya shughuli zao za sanaa, ambalo kutakuwa na kila kitu kwa maana ya vifaa vyote muhimu vitakavyohitajika kuandaa kazi zao za filamu.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by HABARILEO (@habarileo_tz)

Jambo lingine, amesema wamejifunza namna ya kujitambua na kujipa thamani kama wasanii, huku akisema mtu akimuhitaji kwa upande wake lazima amtajie maeneo yenye hadhi za juu kwa ajili ya kukutana.

 

Habari Zifananazo

Back to top button