WFP yasitisha shughuli zake Goma

GOMA: SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limelazimika kusitisha shughuli zake mjini Goma na eneo kubwa la Kivu Kaskazini.
Katika taarifa kwenye mtandao wa kijamii wa X, WFP ilisema ameamua kuchukua hatua hiyo kutokana na kuongezeka kwa ghasia.
“Watu 800,000 katika eneo la Kivu Kaskazini wanategemea msaada muhimu wa chakula na lishe”. WFP ilisisitiza.SOMA: WFP waikabidhi serikali kituo msaada wa chakula
WFP itarejelea shughuli zake wakati hali itakapotengamaa kwa jamii na wafanyakazi wake.
Operesheni za WFP katika maeneo mengine ya DR Congo zitaendelea kama kawaida.



