WHO yaahidi vifaa tishio la Ebola

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO), limeahidi kushirikiana na serikali ya Tanzania kwa kutoa  vifaa vya kutosha  vya  matayarisho muhimu ya kudhibiti viashiria vya tishio la ugonjwa wa Ebola.

Mtaalam wa Maabara wa Shirika la Afya (WHO) nchini, Mura Ngoi, akizungumza   na waandishi wa habari mkoani hapa jana Septemba 3,2022, alisema wameainisha mikoa inayohitaji mahitaji muhimu ya msaada, nguvu kazi na vitendea kazi kwa ajili ya kukinga, kudhibiti kuingia na kuenea kwa ugonjwa huo.

Ngoi  amesema WHO kwa kushirikiana na serikali na kwa uzoefu wao  katika nchi nyingine zenye ugonjwa huo, ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Uganda, imejipanga katika kusaidia kifedha na vitendea kazi kudhibiti viashiria vya ugonjwa huo nchini.

Amesema kwa kushirikiana na Wizara ya Afya wanatoa mafunzo kwa watumishi wa afya mkoani humo katika kupambana na viashiria vya ugonjwa huo.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x