WHO yasikitishwa kusitishwa kwa ufadhili wa HIV

MAREKANI: SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limeonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu athari za kusitishwa mara moja kwa ufadhili wa programu za HIV katika nchi za kipato cha chini na cha kati.

Programu hizi zimekuwa na manufaa makubwa kwa zaidi ya watu milioni 30 duniani kwa kuwapatia tiba ya kuokoa maisha kwa wale wanaoishi na virusi vya HIV.

Kwa mujibu wa takwimu za WHO za mwaka 2023 zinaonyesha kuwa watu zaidi ya milioni 39 wanaishi na virusi vya HIV duniani. SOMA: Wizara yapokea msaada mapambano ya Ukimwi

WHO imesema kusitishwa kwa ufadhili wa programu hizi kutawaweka watu  wanaoishi na virusi vya Ukimwi  hatarini  zaidi na kusababisha ongezeko kubwa la vifo  kama ilivyokuwa awali katika miaka ya 1980, maelfu ya watu walikufa ikiwemo Marekani.

Shirika la Afya Duniani limesisitiza umuhimu wa kuendelea na programu hizi ili kuepusha athari mbaya na kudumisha mafanikio yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya HIV.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button