Wizara kujenga vituo ubunifu wa teknolojia

DSM; WIZARA ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, imejipanga kujenga vituo vya ubunifu katika teknolojia itakayowezesha vijana mbalimbali kuzitumia kuboresha kazi zao za kibunifu.

Imesema kwa kuanzia itaanza na mikoa ambayo ni Dar es Salaam, Dodoma, Lindi,Tanga, Mwanza, Mbeya na Zanzibar.

Mkurugenzi wa Huduma za TEHAMA, Mohamed Mashaka amesema hayo leo Dar es Salaam katika mkutano wa saba wa TEHAMA, ulioandaliwa na Tume ya Tehama nchini (ICTC). Mkutano huo ulijikita kujadili mchango wa TEHAMA kwa vijana pamoja na changamoto mbalimbali wanazokubaliana nazo.

Amesema vituo hivyo vitajengwa katika maeneo ya shule ambavyo vitasaidia vijana nchini kuendelea kuibua vitu mbalimbali vinavyuohusiana na teknolojia pamoja na kuendeleza.

Amewaomba wadau mbalimbali kushirikiana katika kuanzisha vituo hivyo, lengo likiwa ni kukuza vipaji tofauti.

Pia alisema Wizara hiyo ina mpango wa kujenga minara pembezoni mwa nchi katika mikoa ambayo imekuwa na shida ya kupata mitandao ya intanent.

Amesema mpango huo ni kuwezesha minara yenye nguvu ya kiwango cha kutoka 2G kwenda 3G na zaidi, Ili kuwezesha wananchi kutumia simu janja za mikononi na kuweza kufikia fursa mbalimbali ikiwemo kujifunza kuhusu teknolojia ibukizi.

Aidha amesema Wizara pia inatengeneza sera hususani ya vijana haswa walio wabunifu Ili waweze kuhudunu katika mabafiliko ya teknolojia ambayo pia itaenda mbali kuwezesha kuwa na vipaji katika masuala ya teknolojia.

Mkurugenzi Mkuu wa ICTC, Dk Nkundwe Mwasaga amesema watu wengi wamekuwa na hofu na akili bandia kwamba inaweza kuwakosesha kazi, jambo ambalo sio kwani inaleta tija na kwamba watu wakipewa ujuzi mpya kuhusu teknolojia hiyo itasaidia.

Kuhusu vijana amesema tume imefadhili vijana 130 kutoka mikoa balimbali, ili kushiriki mkutano kuweza kujifunza mambo mbalimbali kuhusu Tehama na hata mabadiliko ya teknolojia.

Habari Zifananazo

Back to top button