Wizara kutilia mkazo soko la nje mifugo
WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imesema itaendelea kuangalia Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), kwa kuwa ni eneo ambalo likiimarika mifugo iliyopo itaimarika hivyo kuwezesha upatikanaji wa soko la nje ya nchi.
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Riziki Shemdoe amesema hayo alipotembea wakala huo jijini Dar es Salaam.
Profesa Shemdoe amesema katika eneo hilo jitihada zimeonekana kwani miaka michache iliyopita Tanzania ilikuwa inapeleka nyama nje ya nchi tani 1000, lakini hadi mwaka huu wa fedha unapomalizikia imeshavuka tani 12,000, maana yake ni kwamba mifugo ya Tanzania imekuwa ikikidhi soko hilo.
“Kwa hiyo tunakoelekea ni pazuri kwenye kufanya export ya mifugo kitakachotusaidia ni wakala huu kufanya kazi yake vizuri ili kuweza kupata ithibati mbalimbali ambazo zinaweza kutusaidia kusafirisha nyama au mifugo nje ya nchi,”amesema.
Kwa maelezo yake kazi inayofanyika katika wakala huo inasaidia kutambua magonjwa ya mifugo nchini, ili kuweza kuyazuia au kuyaondoa kabisa.
Pia kazi nyingine ni utengenezaji wa chanjo mbalimbali zinazosaidia kufanya mifugo isiambukizwe au isipate magonjwa mbalimbali.
“Hapa kuna maabara zenye vifaa vya kisasa, na Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo ambazo zimesaidia kuongeza vifaa na kusaidia kubadilisha baadhi ya maabara ili ziweze kuwa kisasa zaidi,”amesema.
Kutokana na jitihada mbalimbali zinazofanyika katika wakala huo aliupongeza uongozi pamoja na madaktari wote kwa kazi nzuri inayofanyika.
Naye Mtendaji Mkuu wa wakala huo, Dk Stella Bitanyi ameshukuru kwa ujio huo wa Katibu Mkuu ambao umemwezesha kuzifahamu shughuli mbalimbali wanazozifanya.
“Kama wakala tutafanya kazi kwa weledi zaidi ili kuipeperusha vema bendera ya wizara yetu katika udhibiti wa magonjwa ya mifugo,” amesema.
Amesema ni mategemeo kuwa ziara hiyo ya Profesa Shemdoe itazaa matunda kwa kuwa amezifahamu kazi zao hivyo amejua uwezo walionao wa kutambua magonjwa ya mifugo nchini, uwezo walionao wa uzalishaji wa chanjo na utambuzi wa ubora wa chanjo, uwezo walionao kwenye usajili na udhibiti wa ubora wa viuatilifu vya mifugo , lakini uwezo walionao kwenye tafiti na kuboresha vyakula vya mifugo nchin